KOCHA NDANDA KUVUNJA MWIKO VPL

KOCHA NDANDA KUVUNJA MWIKO VPL

606
0
KUSHIRIKI

NA WINFRIDA MTOI

KOCHA wa Ndanda, Malale Hamsini, ni kama amechoshwa na kitendo cha kikosi chake kuwa katika kundi la timu za kushuka daraja kila msimu na sasa anataka kuvunja mwiko msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL).

Huu ni msimu wa nne kwa Ndanda kushiriki ligi hiyo na katika misimu miwili mfululizo iliponea chupuchupu kushuka daraja.

Lakini kocha huyo, amesema wamejipanga kumaliza moja ya nafasi tano za juu katika msimamo wa ligi hiyo, inayoshirikisha timu 16 zinazowania ubingwa msimu huu.

Akizungumza na BINGWA jana, Malale alisema pamoja na ugumu wa ligi hiyo, amejiwekea malengo makubwa ya kukipigania kikosi chake kufanya vizuri ili kuepuka kuwamo kwenye kundi la timu zinazoshuka daraja.

“Ndanda imekuwa ikimaliza ligi nafasi ambayo hairidhishi, lakini msimu huu tumejipanga kupambana kuhakikisha hatubanduki moja ya nafasi tano za juu.

Kwa sasa kinachoniumiza kichwa ni safu yangu ya ushambualiaji, kwani naisuka vilivyo ili kuhakikisha inafunga mabao mengi inavyowezekana, naamini nitafanikiwa kwa sababu vijana wangu ni waelewa,” alisema kocha huyo.

Ndanda inashika nafasi ya nane katika msimamo wa ligi hiyo kutokana na pointi saba baada ya kucheza michezo mitano na kushinda miwili, wakitoka sare katika  mchezo mmoja na kupoteza miwili.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU