MECHI ZA WIKIENDI HII KUZIOKOA ARGENTINA, UHOLANZI, ‘SAUZI’?

MECHI ZA WIKIENDI HII KUZIOKOA ARGENTINA, UHOLANZI, ‘SAUZI’?

469
0
KUSHIRIKI
Netherlands' defender Ron Vlaar (L) and Argentina's forward and captain Lionel Messi vie for the ball during the semi-final football match between Netherlands and Argentina of the FIFA World Cup at The Corinthians Arena in Sao Paulo on July 9, 2014. (Fabrice Corrrini/Getty Images)

WIKIENDI hii hakutakuwa na mechi za Ligi Kuu barani Ulaya na badala yake kutakuwa na zile za kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia za mwakani nchini Urusi.

Mpaka kufikia Oktoba 10 mwaka huu, kutakuwa na si chini ya timu 13 zitakazoungana na Brazil, Iran, Japan, Mexico, Ubelgiji, Korea Kusini, Saudi Arabia na wenyeji Urusi, ambazo zimeshafuzu.

Fainali hizo zinazosimamiwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), zinatarajiwa kuanza Julai mwakani mjini Moscow.

Hata hivyo, haya ni maswali yanayosubiri majibu kuelekea michuano hiyo mikubwa kwenye ulimwengu wa soka.

Argentina

Mara kadhaa Argentina wamewahi kuwa hatari kuzikosa fainali hizo. Mwaka 1993, waliokolewa na bao la Diego Maradona katika mchezo wa kufuzu dhidi ya Australia. Mwaka 2010, huenda wasingekwenda Afrika Kusini kama si bao la dakika za majeruhi la Mario Bolatti.

Endapo Argentina watafungwa na Peru kesho, basi washindi hao mara mbili wa Kombe la Dunia watakuwa hatarini zaidi ya kutokwenda Urusi na itakuwa ni mara yao ya kwanza kutocheza michuano hiyo tangu mwaka 1970.

Afrika Kusini ‘Sauzi’

Kikosi cha Bafana Bafana kimekuwa kwenye wakati mgumu katika mechi za kufuzu kwani kimefungwa michezo yote miwili dhidi ya Cape Verde.

Hata matokeo ya mechi yao waliyoshinda mabao 2-1 dhidi ya Senegal yamefutwa na Fifa kwa madai kwamba mchezo huo utarudiwa baada ya uchunguzi kubaini mwamuzi, Joseph Lamptey, alikuwa amepanga matokeo.

Hatari nyingine ya Afrika Kusini katika Kundi D ni kiwango kizuri cha Burkina Faso kwa sasa. Burkina Faso watakuwa kwenye nafasi nzuri ya kucheza Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza katika historia ya taifa hilo endapo wataichapa Bafana Bafana Jumapili hii.

Uholanzi

Si Argentina pekee iliyo hatarini ya kutokwenda Urusi, bali balaa hilo linaihusu pia Uholanzi ambayo hata mwaka jana ilishindwa kushiriki fainali za Euro.

Uholanzi imekuwa ikiyumba na hiyo ilikuwa sababu kubwa ya kufukuzwa kazi kwa kocha Danny Blind na kibarua hicho kukabidhiwa kwa Dick Advocaat ambaye hii ni mara yake ya tatu kuinoa timu hiyo.

Hata kama Waholanzi watashinda mchezo wao wa Jumamosi dhidi ya Belarus, watalazimika kuwaombea Luxembourg waishangaze dunia kwa kuwafunga Sweden.

Marekani

Marekani hawajaikosa michuano ya Kombe la Dunia kwa awamu tatu zilizopita na zote hizo walikuwa wanamaliza mechi za kuwania kufuzu wakiwa kileleni.

Hata hivyo, hadithi inaweza kuwa tofauti katika safari yao ya mwaka huu ya kuiwania tiketi ya kwenda Urusi, ikizingatiwa kuwa imeshapoteza mechi zake mbili zilizopita dhidi ya Mexico na Costa Rica.

Wikiendi hii, kikosi hicho cha mkufunzi wa kimataifa wa Ujerumani, Jurgen Klinsmann, kitacheza na Panama ambao pia wameonekana kuipania michuano ya Urusi ambayo itakuwa ya kwanza katika historia ya soka la nchi yao.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU