MNENE MAKWETA AMVULIA KOFIA SHUSHO

MNENE MAKWETA AMVULIA KOFIA SHUSHO

234
0
KUSHIRIKI

NA MWANDISHI WETU

RAPA kutoka kundi la Machalii wa Yesu la jijini Arusha, Mnene Makweta, ameweka wazi jinsi anavyomkubali mkongwe wa muziki wa Injili nchini, Christina Shusho, kwa kuufanyia kava wimbo wake wa Umenifanya Ning’are.

Mnene ameliambia Papaso la Burudani kuwa ameamua kuurudia wimbo huo maarufu kwa kupitisha michano yake ambayo itazidi kuupaisha wimbo huo na kuonyesha heshima yake kwa Christina Shusho.

“Wimbo nauachia kesho Ijumaa, Shusho ni mwimbaji ambaye namkubali ndiyo maana nimeamua niufanyie kava wimbo wake ambao bila shaka utazidi kuwabariki mashabiki wa gospo nchini,” alisema Makweta.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU