NYOSHI, TUNDA MAN KUMTOA MISS SINZA KESHO

NYOSHI, TUNDA MAN KUMTOA MISS SINZA KESHO

231
0
KUSHIRIKI

WINFRIDA MTOI NA TIMA SIKILO

WAREMBO 10 wanatarajiwa kuchuana vikali katika shindano la kusaka taji la Kitongoji cha Sinza, litakalofanyika kesho kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Denfrance uliopo Sinza White Inn, jijini Dar es Salaam.

Watakaoshuka jukwaani kuwania taji hilo ni Veronica Anastazi (19), Ackey Seme (19), Jesca Elias (21), Jackline Makala (22), Lisa Meswin (18), Sofia Mndamshim (24), Irene Mwelelo (23), Shubila Kaigarula (21), Elice Ernest (23) na Rehema (18).

Wasanii watakaotoa burudani kusindikiza shindano hilo ni msanii wa Bongo Fleva, Tunda Man, Bendi ya El- Classico ya Nyoshi El Sadaat na Bendi ya Santon Sound ikiongozwa na waimbaji Mackey Fanta na Tabia  Batamwanya aliyewahi kuwa Miss Singida.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mratibu wa shindano hilo, Nasib Mahinya, alisema  zawadi kwa mshindi wa kwanza itakuwa Sh 100,000, kiasi  hicho atapewa mshindi wa pili na tatu huku washiriki wengine watapata kifuta jasho Sh 50,000.

“Zawadi zinaweza kuongezeka kwani kuna wadhamini wameonyesha nia ya kutusapoti. Lakini pia kuna taji la Balozi wa New Habari 2006 (Ltd), litakalotolewa na kampuni hiyo ambao ni wadhamini wakuu wa shindano letu,” alisema Mayinya.

Katika hatua nyingine, Mwakilishi wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, inayochapisha magazeti ya Mtanzania, Bingwa, Dimba na Rai, Michael Maurus, alisema watachukua mshiriki mmoja atakayekuwa balozi wa kampuni hiyo.

Alisema balozi huyo atakuwa anashiriki kwenye shughuli mbalimbali za kampuni, ikiwamo kutangaza magazeti hayo kwa kipindi cha mwaka mmoja.

“Sisi ni wadau wa urembo, tumeamua kudhamini tena Miss Sinza mwaka huu kama tulivyofanya mwaka jana kwa sababu tunajua changamoto ya sasa kwa  mashindano haya ni udhamini,” alisema.

Viingilio katika shindano hilo kitakuwa  ni Sh  30,000 kwa VIP  na Sh 10,000.

Mbali ya New Habari, wadhamini wengine wa shindano hilo ni Clouds Media, Denfrance Hotel, Tambaza Auctional Mart, CXC Africa, La Challz Pub, Green Palm Resort, Integrated Communication, 3D Beauty & Decollation, Nguzo Entrepreneurs, Ultimate Security, Big Solution na Event Light.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU