RIBERY APEWA ZA USO NA BABBEL

RIBERY APEWA ZA USO NA BABBEL

412
0
KUSHIRIKI

MUNICH, Ujerumani

MKONGWE wa Bayern Munich, Markus Babbel, amemjia juu staa Franck Ribery, akiwaambia hata siku moja asijilinganishe na wakali Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.

Ribery yuko nje ya uwanja akiuguza majeraha yake ya goti aliyoyapata katika mchezo wa Bundesliga dhidi ya Hertha Berlin na amekuwa akitajwa kuhusika katika sakata la kufukuzwa kazi kwa kocha Carlo Ancelotti.

Ancelotti alitimuliwa baada ya kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa PSG, mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya ambao Ribery na Arjen Robben, hawakuingia ‘first eleven’ ya Mwitalia huyo.

Kwa upande wake, Babbel amekerwa na kitendo cha Ancelotti kufukuzwa na anaamini Ribery mwenye umri wa miaka 34 alichangia kwa kiasi kikubwa.

“Franck Ribery hajafunga hata bao moja Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa miaka miwili iliyopita. Anajiona kama Cristiano Ronaldo au Lionel Messi. Lakini ukweli si hivyo. Ukweli ni kwamba hajawafikia,” alisema Babbel alipokuwa anahojiwa na kituo cha televisheni cha Sky 90.

Ribery alitupa jezi yake wakati alipoitwa benchi kwenye mchezo mwingine wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Anderlecht. “Hii kwangu haikubaliki,” alisema Babbel ambaye alishinda mataji matatu ya Bundesliga,” alisema.

Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu baada ya kuumia goti katika mchezo wa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Hertha Berlin.

 

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU