VANESSA MDEE ALAMBA DILI LA UBALOZI

VANESSA MDEE ALAMBA DILI LA UBALOZI

405
0
KUSHIRIKI

NA MWANDISHI WETU

WAKATI akijiandaa kutumbuiza kwa mara ya kwanza ndani ya Mkoa wa Njombe katika tamasha la Fiesta litakalofanyika kesho kwenye viwanja vya Sabasaba, msanii Vanessa Mdee amepata dili la kuwa balozi wa Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro iliyopo jijini Dar es Salaam.

Staa huyo wa singo ya Kisela, ametangaza kuwa balozi wa hoteli hiyo ya kifahari kupitia ukurasa wake wa Instagram baada ya Bosi wa Hyatt Kilimanjaro, Nicolas Cedro, kuweka picha inayomwonyesha V Money akidondosha wino (akiweka saini) kwenye mikataba.

“Great to have Vannesa Mdee dropping into my Hyatt Kilimanjaro office, we look forward to working with you,” aliandika Garry, mmoja wa wadau muhimu kwenye hoteli hiyo akithibitisha ubalozi mpya wa Vanessa Mdee.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU