FAIZA ALLY HAJAIACHA SALAMA MICHEPUKO

FAIZA ALLY HAJAIACHA SALAMA MICHEPUKO

692
0
KUSHIRIKI

NA KYALAA SEHEYE

MWANAMITINDO na mjasiriamali maarufu kwenye mitandao ya kijamii, Faiza Ally, hajaiacha salama michepuko inayoiba waume za watu kwani imekuwa chanzo kikubwa cha matatizo katika ndoa nyingi.

Faiza ambaye ni mzazi mwenza na mkongwe wa muziki wa hip hop nchini (Joseph Mbilinyi ‘Sugu), amelidokeza Papaso la Burudani kuwa mchepuko unapompenda mume wa mtu hujaribu kuwa na adabu na si kumwonyesha dharau mpaka kwa mke halali.

“Kama unapenda kuonyesha mwanamume wako ni bora utafute ambaye hajaoa, sasa kama unachukua mume wa mtu halafu unakosa adabu, unakuwa na kiburi ambacho kakikusaidii halafu mwisho wa siku unaambulia maumivu ya kuachwa,” alisema Faiza Ally hivi karibuni katika sherehe ya 40 ya mtoto wake wa pili, Lil Jr.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU