REUS ASEMA MAJERAHA YATAMFILISI

REUS ASEMA MAJERAHA YATAMFILISI

372
0
KUSHIRIKI

MUNICH, Ujerumani

MPACHIKAJI mabao hatari wa Borussia Dortmund, Marco Reus, amesema yuko tayari kutumia utajiri wake wote ili apone kabisa majeraha.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28, amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara na baada ya kuumia mwishoni mwa msimu uliopita, anatarajiwa kurejea dimbani mwanzoni mwa mwaka ujao.

Reus amefichua kuwa amekuwa akiumizwa na maumivu ya mara kwa mara na angetumia kiasi chochote ili kuwa fiti.

“Tukiwa kama wachezaji wakubwa, huwa tunaingiza fedha nyingi, lakini huwa tunatumia mpunga mrefu kwa ajili ya afya zetu. Ninaweza kutumia fedha zote nilizonazo ili nipone, niweze kufanya kazi yangu. Kufanya kile ninachokipenda, yaani kucheza soka,” alisema Mjerumani huyo.

Staa huyo amekuwa kwenye kikosi cha Dortmund tangu alipojiunga nayo mwaka 2012 akitokea Borussia Monchengladbach.

Kwa upande mwingine, amesema anatazamia kuikacha Dortmund na kutimkia kwingineko pindi mkataba wake utakapomalizika mwaka 2019.

“Kuna klabu nne au tano zinanitaka. Mei 31 mwaka ujao, nitakuwa na umri wa miaka 30. Huo utakuwa ndio mkataba wangu mnono wa mwisho na nafasi ya mwisho kujaribu kufanya kitu tofauti.

“Natakiwa kuwa muwazi kuwa sijui nitatua wapi. Kwa sasa, nafurahia kuwa Dortmund na sifikirii kitakachotokea mwaka 2019. Lakini ni kweli, muda utafika na nitakaa na kufanya uamuzi makini,” alisema Reus.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU