SHILOLE, CHAMELIONE JUKWAA MOJA UINGEREZA

SHILOLE, CHAMELIONE JUKWAA MOJA UINGEREZA

448
0
KUSHIRIKI

NA CHRISTOPHER MSEKENA

MSANII wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, amesema yupo nchini Uingereza kwa ajili ya ziara yake ya muziki itakayomkutanisha jukwaa moja na mwanamuziki mahiri wa Uganda, Jose Cha Chameleone.

Akizungumza na Papaso la Burudani, Shilole alisema ziara hiyo ya Uingereza ndiyo sababu kubwa iliyofanya asitumbuize kwenye tamasha la Fiesta linaloendelea mwishoni mwa wiki hii Nyanda za Juu Kusini.

“Kesho tuna shoo kubwa pale Amsterdam, kutoka Afrika nitakuwa mimi na Jose Chameleone, natarajia kufanya vizuri kama kawaida yangu, baada ya hapo ndiyo ntarudi Bongo,” alisema Shilole.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU