KIUNGO MTIBWA KUIKAZIA MISULI SIMBA

KIUNGO MTIBWA KUIKAZIA MISULI SIMBA

1731
0
KUSHIRIKI

NA MARTIN MAZUGWA

KIUNGO wa Mtibwa Sugar, Mohamed Issa ‘Banka’, amesema baada ya kutimiza majukumu yake katika kikosi cha Taifa Stars, sasa anajiweka fiti ili kuikabili Simba.

Mtibwa Sugar inatarajia kucheza na Simba katika mchezo utakaopigwa Jumapili kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

Tayari kiungo huyo amekiongoza kikosi chao kushinda michezo mitatu na kutoka sare mbili, huku kikishika nafasi ya pili kutokana na pointi 11 ilizopata sawa na Azam na Simba, ambao wapo kileleni kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Akizungumza na BINGWA juzi, Issa alisema atatumia muda huu wa wiki nzima kujiweka fiti ili kuipigania timu yake kuibuka na ushindi dhidi ya Simba.

“Nipo Mtibwa Sugar kwa kazi moja ya  kuhakikisha timu inafanya vizuri zaidi na kurejesha heshima yake ya miaka ya nyuma,” alisema  Issa.

Issa alisema hatishwi na nyota wa Simba, kwani atahakikisha anaisaidia timu yake kuondoka na pointi tatu zitakazowafanya wakae kileleni.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU