MAYANGA KUWAANDALIA AKINA OKWI MECHI MBILI

MAYANGA KUWAANDALIA AKINA OKWI MECHI MBILI

1968
0
KUSHIRIKI

NA SALMA MPELI

KOCHA wa Taifa Stars, Salum Mayanga, amesema anahitaji mechi mbili za kirafiki za kimataifa ili aweze kushinda dhidi ya Uganda ‘The Cranes’, katika mechi ya kuwania kufuzu fainali za Afrika (AFCON) zitakazopigwa mwaka 2019 nchini Cameroon.

Taifa Stars inatarajia kucheza na Uganda Machi mwakani, inayoundwa na mshambuliaji wa nchi hiyo, Emmanuel Okwi, anayechezea kikosi cha Simba.

Katika mchezo wa kwanza uliopigwa Juni mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex, jijini Dar es Salaam, Taifa Stars ilitoka sare ya kufungana bao 1-1 na Lesotho.

Kutokana na matokeo hayo, Mayanga alisema anahitaji kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa Novemba mwaka huu, kujiandaa na Uganda.

Akizungumza na BINGWA juzi, Mayanga alisema baada ya kutoka sare ya kufungana bao 1-1 na Malawi katika mechi ya kirafiki iliyochezwa juzi kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini, nguvu yake anaielekeza kwenye Afcon.

Mayanga alisema anahitaji kupata mechi hizo kabla ya kuwavaa Uganda, ili aweze kurekebisha makosa yaliyojitokeza kwenye kikosi chake.

Alisema anaendelea kukijenga kikosi chake kwa kufanya mabadiliko zaidi ili kupata matokeo mazuri katika michuano hiyo ya Afrika.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU