MZAMIRU ATAJA SABABU ZA KUPEWA KADI NYEKUNDU

MZAMIRU ATAJA SABABU ZA KUPEWA KADI NYEKUNDU

2392
0
KUSHIRIKI

NA WINFRIDA MTOI

KIUNGO wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mzamiru Yassin, ameweka wazi sababu ya yeye kupewa kadi nyekundu kuwa ni kutokana na wachezaji wa Malawi kuingia uwanjani wakiwa wamepania kulipa kisasi kwa Tanzania.

Hali hiyo ilitokana na Taifa Stars kuwafunga Malawi mabao 2-0 katika michuano ya Cosafa iliyofanyika Juni mwaka huu, nchini Afrika Kusini na Mzamiru alikuwa miongoni mwa wachezaji waliokuwa kwenye kikosi hicho.

Akizungumza na BINGWA juzi baada ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, Mzamiru alisema wapinzani wao waliingia uwanjani wakiwa na hasira za kulipa kisasi cha Afrika Kusini.

Alisema licha ya kuwa Malawi walikuwa wazuri lakini uchezaji wao ulikuwa mbaya, kwani ilionekana walikuwa wamejipanga kufanya lolote uwanjani ili kupata ushindi waweze kulipa kisasi cha mabao 2-0 waliyowafunga Cosafa.

“Timu ya Malawi ni nzuri lakini jinsi walivyokuwa wanacheza leo (juzi), ilionekana walikuwa wapepania mchezo kwa ajili ya kulipa kisasi, hata kadi niliyopewa mimi sikuitegemea na nilishangaa mwamuzi alifanya hivyo kwa sababu ila ni mambo ya mchezo umeisha tunajipanga na mechi nyingine,” alisema.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU