ALI KIBA RASMI KUTUMBUIZA TUZO ZA AFRIMA NIGERIA

ALI KIBA RASMI KUTUMBUIZA TUZO ZA AFRIMA NIGERIA

1493
0
KUSHIRIKI

NA CHRISTOPHER MSEKENA

MFALME wa Bongo Fleva, Ali Kiba, ametangazwa rasmi kuwa mmoja ya wanamuziki watakaoshiriki kujenga historia mpya ya burudani barani Afrika kwa kutumbuiza kwenye sherehe za tuzo za All Africa Music Awards (Afrima 2017) zitakazoambatana na tamasha la muziki la siku tatu huko Lagos, Nigeria.

Mbali na kutumbuiza staa huyo wa singo ya Seduce Me, ni miongoni mwa wasanii sita wa Tanzania waliochaguliwa kuwania tuzo hizo za mwaka huu zinazotarajia  kuanza kutolewa Novemba 10 hadi 12 mwaka huu kwenye ukumbi wa Host City, Lagos Nigeria.

Wasanii wengine wa Bongo Fleva ambao wapo kwenye vipengele tofauti vya tuzo za Afrima mwaka huu ni Vanessa Mdee, Diamond Platnumz, Nandy, Msafiri Zawose na Lady Jay Dee.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU