CHEKI YALIYOITEKA BALLON D’OR 2017

CHEKI YALIYOITEKA BALLON D’OR 2017

1044
0
KUSHIRIKI

LONDON, England

UKIIANGALIA orodha ya nyota 30 waliochaguliwa kuwania tuzo ya Ballon d’Or mwaka huu, ni sawa na kusema itakuwa vita ya wakali wote, kwani takribani majina ya wachezaji wote wakubwa yapo mule.

Ingawa sio kitu cha kushtusha sana kusikia majina kama Cristiano Ronaldo, Lionel Messi, Neymar, Luis Suarez, Gianluigi Buffon, Sergio Ramos na Kylian Mbappe yakiwemo kwani tuzo hiyo ni kubwa duniani kwa wachezaji binafsi.

Hata hivyo, katika kutazama orodha hiyo yamegundulika mambo matano ambayo hukuweza kuyang’amua haraka.

Wapya kibao

Ni hali ya kushangaza ambapo zaidi ya nusu ya nyota 30 waliokuwepo kwenye orodha ya mwaka jana wameshindwa kuingia mwaka huu.

Nyota hawa 17 ndio waliokuwepo kwenye orodha iliyotoka miezi 12 iliyopita lakini mwaka huu wameonekana si lolote: Sergio Aguero (Man City / Argentina), Gareth Bale (Real Madrid /Wales), Diego Godin (Atletico/Uruguay), Gonzalo Higuain (Juventus /Argentina), Zlatan Ibrahimovic (Man United /Sweden), Andrés Iniesta (Barcelona / Hispania), Koke (Atletico / Hispania), Hugo Lloris (Tottenham / Ufaransa), Riyad Mahrez (Leicester / Algeria), Thomas Müller, Manuel Neuer (Bayern/ Ujerumani), Paul Pogba (Man United / Ufaransa), Rui Patricio (Sporting /Ureno), Jamie Vardy (Leicester /England), Arturo Vidal (Bayern /Chile).

Madrid noma aisee

Takribani asilimia 23 ya nyota hao 30 (wachezaji saba) ni kutoka katika klabu ya Real Madrid; Karim Benzema, Cristiano Ronaldo, Isco, Toni Kroos, Marcelo, Luka Modric na Ramos.

Na hakuna timu nyingine ambayo ina wachezaji zaidi ya watatu kwenye orodha hiyo zaidi ya PSG, ambao wana Edinson Cavani, Mbappe na Neymar

Edin Dzeko naye yumo!

Wengi watashtushwa kuliona jina la straika huyo huku wachezaji wengine wakali zaidi yake pengine wakiachwa. Hii ni mara ya kwanza kwa mpachika mabao huyo wa Roma kuchaguliwa baada ya miaka nane, mara ya mwisho alichaguliwa mwaka 2009 akiwa Wolfsburg.

Mbappe kiboko

Staa huyo wa PSG ameingia kwenye orodha hiyo akiwa na umri mdogo zaidi, miaka 18 na miezi tisa, na kuivunja rekodi ya straika wa zamani wa Liverpool, Michael Owen, aliyoiweka mwaka 1998.

Ufaransa wamekomesha

Kuna mataifa 17 tofauti baina ya majina hayo 30. Lakini cha kushangaza Ufaransa imezidisha idadi ya wachezaji wao kuliko taifa lolote ambapo kuna majina manne; Benzema, Griezmann, Kante na Mbappe. Huku mataifa yanayofuata yakiwa ni Argentina, Ubelgiji, Brazil na Hispania zenye wachezaji watatu kila moja.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU