FELISTA KIDUU AACHIA ‘NALINDWA NA NGUVU ZA MUNGU’

FELISTA KIDUU AACHIA ‘NALINDWA NA NGUVU ZA MUNGU’

242
0
KUSHIRIKI

Na MWANDISHI WETU

MWIMBAJI mpya wa nyimbo za Injili kutoka jijini Arusha, Felista Kiduu, ameachia wimbo wake mpya unaoitwa Nalindwa na Nguvu za Mungu akiwa amemshirikisha Daniel Isingo.

Akizungumza na Papaso la Burudani, Felista aliwaomba mashabiki wa gospo nchini kumpokea na kumuunga mkono katika huduma yake changa ya uimbaji ukizingatia ndiyo kwanza ameanza.

“Nimeanza kuachia audio baadaye video itafuata, nawaomba mashabiki wa muziki wa Injili wautafute wimbo huu kwenye mitandao ya kijamii ili waweze kuusikiliza ujio wangu wa pili, naomba sapoti yao,” alisema Felista.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU