MAJERUHI MANE KUSUGUA BENCHI WIKI SITA

MAJERUHI MANE KUSUGUA BENCHI WIKI SITA

399
0
KUSHIRIKI

LONDON, England

KLABU ya Liverpool imebainisha kuwa straika wao, Sadio Mane, anaweza kukosa wiki sita zijazo msimu huu kutokana na majeraha ya misuli.

Mane alipata majeraha akiwa na timu ya Taifa ya Senegal ambayo mwishoni mwa wiki iliyopita iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Visiwa vya Cape Verde.

“Sadio Mane hataweza kucheza baada ya kupata majeraha ya misuli katika majukumu ya kimataifa, Liverpool inathibitisha,” taarifa hiyo inasomeka kwenye tovuti rasmi ya klabu.

“Winga huyo alitolewa mchezoni dakika ya 89 katika ushindi wa Senegal wa 2-0 kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Visiwa vya Cape Verde Jumamosi. Na sasa imethibitika kuwa amepata majeraha katika mechi hiyo ambayo yatamweka nje ya dimba kwa muda usiopungua wiki sita.”

Mane amefunga mabao matatu Ligi Kuu Uingereza katika mechi nne alizocheza akiwa na Reds mwanzo wa kampeni za msimu wa 2017-18.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU