MWAMUZI ADUI WA MOURINHO KATIKATI YA UWANJA

MWAMUZI ADUI WA MOURINHO KATIKATI YA UWANJA

952
0
KUSHIRIKI

MERSEYSIDE, Liverpool

NI wazi taarifa za kwamba mwamuzi, Martin Atkinson, atakuwa katikati mwa wanaume 22 wa Liverpool na Man United wikiendi hii, hazitapokelewa vizuri na Jose Mourinho. Unajua kwanini? Sikia hii.

Atkinson, mwenye makazi yake mitaa ya Bradford, Yorkshire Magharibi, England, alikuwa mwamuzi kwenye mtanange wa ufunguzi Ligi Kuu England baina ya Red Devils hao na West Ham, lakini mashabiki wa United hawatamsahau kwa ‘alichowatendea’ dhidi ya Chelsea mwaka jana, hasa Mourinho.

Atkinson, alishindwa kumwonesha kadi nyekundu beki David Luiz kwa kitendo chake cha kumkita Fellaini na njumu kwenye goti la mguu wake wa kulia, mechi iliyoishia kwa United kubugizwa mabao 4-0 pale Stamford Bridge.

Mara baada ya mchezo huo dhidi ya vijana hao wa Antonio Conte, Oktoba mwaka jana, Mourinho aliamua kutoa dukuduku lake juu ya Atkinson, maneno ambayo huenda tukayasikia tena mara baada ya mchezo wa keshokutwa kutoka kwake, inategemea na matokeo pia.

Mourinho alizungumza kuhusu Atkinson kushindwa kumtoa nje David Luiz, akisema: “Kuna muda unatamani usikie jina la mwamuzi aliye thabiti akiteuliwa kuchezesha mechi kama hizi.

“Hii (dhidi ya Chelsea) ilikuwa ni mechi kubwa kwa pande zote mbili na matarajio ni kuona maamuzi yanayotolewa ndani ya mechi yawe ya kueleweka na vitu kama hivyo…sijaelewa maamuzi ya leo.

“Sijui hata kwanini ameruhusiwa kuchezesha mechi. Nalazimika kusema kwamba nina hofu kutokana na maamuzi yake kama refa.”

Kwa kuzingatia presha na ukubwa wa mechi ya Jumamosi, hilo neno la mwisho ‘sijui hata kwanini ameruhusiwa kuchezesha mechi. Nalazimika kusema kwamba nina hofu kutokana na maamuzi yake kama refa’, ndilo linalobeba maana nzima ya huenda asiridhishwe na kuteuliwa kwake.

Hata hivyo, Atkinson alikuwepo kwenye mtanange ambao United iliichapa Liver mabao 2-1 mwaka 2015 katika dimba la Anfield, ambapo alimwonesha kadi nyekundu ya halali nahodha wa Liver, Steven Gerrard, sekunde 38 tu baada ya kiungo huyo kuingia akitokea benchi.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU