RAIS PANAMA ATANGAZA SIKU YA MAPUMZIKO

RAIS PANAMA ATANGAZA SIKU YA MAPUMZIKO

223
0
KUSHIRIKI

PANAMA CITY, Panama

RAIS wa Panama jana alitangaza kuwa siku ya mapumziko, baada ya timu ya taifa ya nchi hiyo kufanikiwa kufuzu kwa mara ya kwanza fainali za Kombe la Dunia.

Vijana hao wa Kocha, Hernan Dario Gomez, mwanzo walionekana kama wasingefuzu fainali hizo baada ya  matokeo kuwa 1-1 ikiwa ni baada ya  Costa Rica wakiwa mjini Panama City, kusawazisha ikiwa ni baada ya shuti lililoachiwa na straika wao, Gabriel Torres, kupanguliwa na staa, Johan Venegas, akiipatia Costa Rica bao la kuongoza.

Hata hivyo, bao la ushindi ndilo lilizua utata baada ya mpira kuonekana kutovuka mstari wa lango.

Baada ya matokeo hayo, Rais Juan Carlos Varela, akatuma ujumbe kupitia mtandao wake wa kijamii wa Twitter, akitangaza jana kuwa ni siku ya mapumziko.

“Sauti za watu zimesikika, sherekeheni siku hii ya kihistoria kwa Panama. Kesho (jana) ni siku ya kitaifa,” aliandika kiongozi huyo.

“Ni siku ya kihistoria kitaifa. (Kesho itakuwa ni siku ya mapumziko kwa watumishi wa umma na wafanyakazi wa sekta binafsi,” aliongeza.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU