SIMBA: MTIBWA HAITUUMIZI KICHWA

SIMBA: MTIBWA HAITUUMIZI KICHWA

1041
0
KUSHIRIKI

NA SAADA SALIM

KOCHA Msaidizi wa timu ya Simba, Jackson Mayanja, amesema tayari wamepata dawa ya kuiua Mtibwa Sugar, katika mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya kurejea na mbinu mpya nchini.

Simba wanatarajia kucheza na Mtibwa Sugar keshokutwa katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, ambapo kocha huyo raia wa Uganda amejigamba kuwa alipata dawa ya ushindi  akiwa kwao.

Akizungumza na BINGWA jana, Mayanja alisema akiwa Uganda hakulala, kwani alikuwa akiendelea kufanyia kazi udhaifu walionao  Mtibwa kupitia michezo waliyocheza.

Alisema anatarajia kukaa na bosi wake Mcameroon, Joseph Omog na kumpa ujanja wa kuifunga Mtibwa ili kuhakikisha wanaongeza pointi tatu nyingine baada ya kuifunga Stand United mabao 2-1 katika mchezo uliopita.

Mayanja aliongeza kuwa, kabla hajaondoka nchini alikiacha kikosi kikiwa vizuri, lakini  alihakikisha anayafanyia kazi mapungufu ya Mtibwa ili washinde dhidi yao.

“Tunahitaji ushindi katika mchezo dhidi ya Mtibwa, naamini kila mchezaji anafahamu majukumu aliyopewa na benchi la ufundi,” alisema Mayanja.

Aidha, kocha huyo alieleza kuwa, pia wamewajenga kisaikolojia wachezaji wao ili wafanye vizuri katika mchezo unaowakabili.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU