JESUS: MAN CITY IMENIFANYA KUWA BORA

JESUS: MAN CITY IMENIFANYA KUWA BORA

927
0
KUSHIRIKI

MANCHESTER, England

KUFUATIA kiwango safi alichokionesha wakati timu yake ya Brazil ikiisasambua Chile mabao 3-0 juzi kwa kufunga mabao mawili, straika Gabriel Jesus, amesema klabu yake ya Man City imemsaidia kukinoa vilivyo kiwango chake.

Jesus ni mmoja wa wachezaji waliochangia Brazil kukata tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia kwa kishindo, anajiandaa kuiongoza safu ya ushambuliaji ya City wikiendi hii dhidi ya Stoke.

“Nimeimarika si tu kiuchezaji, bali hata kiakili. Nitaendelea kufanya kile ninachokifanya siku zote, iwe ni Manchester au Brazil. Nina furaha na ninachokionesha kwa watu, lakini nafahamu natakiwa kukimbia, kujituma sana ili nioneshe nastahili kuchaguliwa,” alisema.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU