FALCAO AKIRI ‘KUWATONGOZA’ NYOTA WA PERU

FALCAO AKIRI ‘KUWATONGOZA’ NYOTA WA PERU

906
0
KUSHIRIKI

LIMA, Peru

MSHAMBULIAJI wa timu ya taifa ya Colombia, Radamel Falcao, amekiri madai ya kuwashawishi wachezaji wa Peru wasifunge bao na kuyaacha matokeo yabaki 1-1 kwenye mechi yao ya mwisho ya kufuzu Kombe la Dunia mapema wiki hii.

Falcao alitupiwa lawama kwa kitendo chake cha kuzungumza na wachezaji wa Peru na kuwaambia wasitumie nguvu kufunga bao la pili na sare hiyo ikaipeleka Colombia moja kwa moja Urusi huku Peru ikilazimika kucheza mechi za mchujo dhidi ya New Zealand.

“Tulikuwa tunafahamu kilichokuwa kinaendelea kwenye mechi nyingine, tulicheza na matokeo hayo na ndio maana nilijaribu kuwashawishi na wachezaji wa Peru,” alisema Falcao mara baada ya mchezo huo.

Falcao alionekana kumnong’oneza kitu nyota wa Peru, Renato Tapia, ambaye naye alikiri wazi lakini alikanusha kuwa ni kitu kilichoandaliwa.

“Katika dakika tano za mwisho, Wakolombia walitufuata. Walituambia hali halisi iliyokuwa ikiendelea kwenye mechi nyingine, Falcao aliniambia kuwa sote tulishafuzu (kama msimamo ulivyo), lakini ndio soka,” alisema.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU