KIUNGO MTIBWA AMKUNA BANDA

KIUNGO MTIBWA AMKUNA BANDA

2578
0
KUSHIRIKI

Na SAADA SALIM

BEKI wa zamani wa Simba anayekipiga katika timu ya Baroka FC ya nchini Afrika Kusini, Abdi Banda, amesema anavutiwa na kiungo wa Mtibwa Sugar, Mohammed Issa ‘Mo Banka’ na kueleza kuwa, ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa.

Akizungumza na BINGWA, Banda alisema kiungo huyo hatadumu kwa muda mrefu katika kikosi cha Mtibwa kutokana na uwezo alionao, kwani anaamini lazima ataondoka na kusajiliwa na klabu kubwa nchini na nje ya Tanzania.

Alisema Mo Banka alionyesha uwezo mkubwa katika mazoezi ya timu ya Taifa, Taifa Stars, iliyokuwa ikijiandaa kucheza na Malawi katika mchezo wa kirafiki uliopigwa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Alisema alikuwa akimfuatilia zaidi Mo Banka wakati anafanya mazoezi na kikosi cha Stars na kubaini uwezo wake, ndiyo maana amemtabiria kuwa atafika mbali kutokana na uchezaji wake.

“Nimecheza na viungo wengi hapa nchini, lakini yule dogo yuko vizuri sana, akitulia na kupata mtu makini wa kumsimamia ninaamini hana muda mrefu wa kucheza soka bongo,” alisema.

Aidha, Banda alimtaka asivunjike moyo kwa kutopata namba ya kucheza katika kikosi cha Stars, bali anatakiwa kuwa mvumilivu na kupambana, kwani ipo siku atafanya vizuri.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU