MULLER AMREJESHA ANCELOTTI BAYERN

MULLER AMREJESHA ANCELOTTI BAYERN

1285
0
KUSHIRIKI

MUNICH, Ujerumani

LICHA ya kuwa tayari ameshafukuzwa, jina la kocha Carlo Ancelotti limeendelea kutajwa katika klabu ya Bayern Munich, na safari hii ni straika Thomas Muller.

Muller, raia wa Ujerumani, alisema Ancelotti hapaswi kufanywa mbuzi wa kafara kwa mwenendo mbovu wa Bayern.

Bayern waliamua kumtimua Ancelotti baada ya kikosi hicho kuchapwa mabao 3-0 na PSG, katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kumekuwa na tetesi kuwa, kufukuzwa kwake kulichangiwa na baadhi ya mastaa wa timu hiyo waliotaka aondoke.

“Sehemu kubwa ya mwenendo mbovu (wa Bayern) umesababishwa na timu iliyopo uwanjani. Tunatakiwa kuwa wakweli na si kumfanya Carlo Ancelotti kuwa kisingizio.

Kikosi hicho kinanolewa na mkongwe Jupp Heynckes hadi mwishoni mwa msimu, lakini Muller anaamini mashabiki wasitarajie mabadiliko ya haraka.

“Haitakuwa haraka kuona tukicheza soka la sayari nyingine. Kutakuwa na mechi ambazo kwa hakika watu watatutazama na kutukosoa,” alisema Muller, ambaye pia anatajwa kuwa kwenye orodha ya wachezaji walioshinikiza Ancelotti afukuzwe.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU