MURRAY, DJOKOVIC KUNOGESHA AUSTRALIAN OPEN

MURRAY, DJOKOVIC KUNOGESHA AUSTRALIAN OPEN

238
0
KUSHIRIKI

CANBERRA, Australia

VINARA wa tenisi kwa upande wa wanaume na wanawake, Andy Murray  na  Novak Djokovic   watashiriki michuano ya  Australian Open ambayo itafanyika Januari mwakani.

Mkurugenzi Mkuu wa michuano hiyo,  Craig Tiley, alisema jana kwamba nyota hao watashiriki michuano hiyo, baada ya kuwa nje ya uwanja kutokana na sababu mbalimbali.

Alizitaja sababu hizo kuwa Mwingereza anayeshika nafasi ya kwanza kwa ubora,  Murray, hajaingia uwanjani tangu Julai mwaka huu, baada ya kutenguka kiganja katika mchezo wa robo fainali  ya michuano ya Wimbledon wakati    Djokovic alikuwa na matatizo ya goti.

Tiley alisema nyota hao wawili wataungana na Novak Djokovic  na  Stan Wawrinka.

“Wachezaji wote nyota watakuwapo kwenye michuano hiyo ya  Melbourne,” alisema mkurugenzi huyo.

Wawrinka na  Nishikori, nao walikuwa hawajacheza tangu majira ya joto yaliyopita kwa kile kinachosemekana ni matatizo ya goti na kiungio cha kiganja na mkono.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU