REKODI YA RUVU YAWATISHA SINGIDA UTD

REKODI YA RUVU YAWATISHA SINGIDA UTD

610
0
KUSHIRIKI

NA MAREGES NYAMAKA

REKODI ya kikosi cha Ruvu Shooting kufanya vizuri katika uwanja wao wa nyumbani wa  Mabatini uliopo Mlandizi, Pwani inaonekana  kuwatisha wapinzani wao, Singida United.

Ruvu Shooting wanatarajia kuwa wenyeji wa Singida United katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaopigwa kesho kwenye uwanja huo.

Kikosi cha Ruvu hakijapoteza mechi yoyote katika uwanja wake wa nyumbani, zaidi ya kutoka sare mara nne na kupoteza mchezo mmoja ugenini dhidi ya Simba.

Ruvu walifungua pazia la Ligi Kuu kwa kupata kipigo kikali cha mabao 7-0 dhidi ya Simba katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na waliporejea Uwanja wa Mabatini walitoka sare ya bao 1-1 na Kagera Sugar.

Katika mchezo uliofuata, Ruvu walitoka sare ya bila kufungana na Lipuli FC, wakalazimishwa tena sare ya bao 1-1 na Mtibwa Sugar, kabla ya kupata matokeo kama hayo walipovaana na Njombe Mji.

Akizungumza na BINGWA jana, nahodha msaidizi wa kikosi cha Singida United, Mudathir Yahya, alisema mchezo wa kesho utakuwa mgumu kutokana na rekodi ya wenyeji wao wanapocheza nyumbani.

“Mchezo utakuwa mgumu, lakini tumejiandaa kupambana kuchukua pointi tatu, licha ya wapinzani wetu hawa kuwa miongoni mwa timu ambazo ni vigumu kupoteza nyumbani kulingana na rekodi yao,” alisema Mudathir.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU