BEATRICE KITAULI ANG’AA TUZO ZA XTREEM KENYA

BEATRICE KITAULI ANG’AA TUZO ZA XTREEM KENYA

228
0
KUSHIRIKI

NA CHRISTOPHER MSEKENA

TUZO maarufu za muziki wa Injili nchini Kenya, Xtreem Awards 2017, zimetangaza majina ya waimbaji wa Afrika wanaowania vipengele mbalimbali, ambapo Tanzania inawakilishwa na mwimbaji, Beatrice Kitauli aliyechomoza kwenye vipengele viwili.

Akizungumza na Papaso la Burudani, Kitauli alisema nguvu ya mashabiki imefanya aibuke kwenye vipengele viwili ambavyo ni Kolabo Bora ya Mwaka na Mwimbaji Bora Tanzania.

“Naomba mashabiki zangu wote na wale wanaopenda huduma ya muziki wa Injili isonge mbele wanipigie kura kwa njia rahisi ya meseji, ambapo katika kipengele cha Kolabo Bora unaandika COT 8 unaituma hiyo meseji kwenda namba 22275 na Mwimbaji Bora Tanzania unaandika meseji TAG 4, unatuma kwenda namba 22275,” alisema Kitauli.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU