MSHAIRI WA TANZANIA AMGUSA RAIS WA URUSI

MSHAIRI WA TANZANIA AMGUSA RAIS WA URUSI

680
0
KUSHIRIKI

NA MWANDISHI WETU

RAIS wa Urusi, Vladimir Putin, mwishoni mwa wiki iliyopita aliguswa na mashairi mazuri kutoka kwa msanii wa Ushahiri wa Tanzania, Aisha King, katika hafla ya kufungua tamasha la vijana na wanafunzi lililofanyika jijini Sochi, nchini humo.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi ushairi huo kwa Rais Vladimir Putin, Aisha alitunga mashairi hayo kwa maalumu ya kumshukuru kiongozi huyo kwa kuwa mratibu mkuu wa tamasha hilo ambalo linapendwa na vijana.

“Nimemtungia shairi kwa sababu yeye ndiye mratibu mkuu wa tamasha hili kwa hiyo ushairi huu ni kwa ajili ya shukrani tu,” alisema Aisha ambaye alikuwa mmoja wa wajumbe kutoka Tanzania ambao walihudhuria tamasha hilo.

Awali kabla ya kufungua tamasha hilo, Putin alizungumza na vijana wote ambao walihudhuria na kuwashauri katika masuala mbalimbali ya kimaisha na kimaendeleo.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU