NEY WA MITEGO ATEMA CHECHE

NEY WA MITEGO ATEMA CHECHE

590
0
KUSHIRIKI

NA CHRISTOPHER MSEKENA

MSANII wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘ Ney wa Mitego’, amewaonya wasanii wanaoendekeza matukio (kiki) badala ya kufanya kazi nzuri zitakazokubalika, waache kufanya hivyo kwani wanaua muziki wa kweli.

Ney wa Mitego ambaye hivi sasa yupo kwenye maandalizi ya Tamasha la Nguvu ya Kitaa litakalofanyika Jumamosi hii kwenye viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe, jijiji Dar es Salaam, ameliambia Papaso la Burudani kuwa kiki zimeiua tasnia ya filamu hivyo hazipaswi kuendekezwa.

“Bongo Fleva inaingia shimoni tukiendeleza kiki, watu wanafanya kiki kubwa kuliko muziki wenyewe, muziki umebaki kusindikiza kiki, hakika hatutabaki salama tunapaswa kubadilika,” alisema Ney.

True Boy ameyasema hayo ikiwa ni siku chache baada ya kuibuka kwa utata wa inayodaiwa ndoa kati ya msanii, Dogo Janja na Irene Uwoya, huku wengi wakiamini si ndoa ya kweli bali ni kiki ya ujio mpya wa Keisha wa Tip Top Connection.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU