SERENA GOMEZ, JUSTIN BIEBER KWA RAHA ZAO

SERENA GOMEZ, JUSTIN BIEBER KWA RAHA ZAO

381
0
KUSHIRIKI

NEW YORK, Marekani

WAPENZI Selena Gomez na Justin Bieber, wanaripotiwa kurudiana, baada ya mwimbaji na mchungaji, Carl Lentz, kuwapatanisha.

Taarifa za kurudiana wapendanao hao zimekuja baada ya kuwapo tetesi za kuwa tena na uhusiano wa kimya kimya tangu mwezi uliopita.

Hata hivyo, juzi wapenzi hao waliamua kuweka wazi kuwa mambo  yamemalizika na kwa sasa wao ni kitu kimoja.

“Selena na Justin wamerudiana,” chanzo kimoja cha habari kililiambia jarida la  Us Weekly.

“Pamoja na kuwa katika mvutano, lakini  Selena mara zote alikuwa akimuwazia  Justin. Marafiki zake watakuwa wanashangaa kwa sababu hawakutegemea kama itakuwa hivyo,” kiliongeza chanzo hicho.

Chanzo kingine kilichopo karibu na  Justin kiliuambia matandao wa The Sun Online kwamba, kulikuwapo na kazi kubwa ya kumshawishi staa huyo, lakini mchungaji Carl Lentz, ndiye aliyefanikisha kuwashawishi mpaka wakarudiana.

Wapendanao hao ambao walianza uhusiano wao tangu mwaka 2011 kabla ya kutengana 2014, wanasemekana kuanza kusameheana baada ya  Selena kufanyiwa upasuaji wa moyo majira ya joto yaliyopita.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU