JORDAN ASUKA MIPANGO VIDEO YA UMEINULIWA

JORDAN ASUKA MIPANGO VIDEO YA UMEINULIWA

407
0
KUSHIRIKI

 Na ESTHER GEORGE
BAADA ya kutoa audio ya wimbo wake wa Umeinuliwa, mwimbaji wa Gospo nchini, Jordan Ngassa, amesema ameanza kusuka mipango ya kukamilisha video yake.

Akizungumza na Papaso la Burudani, Ngassa alisema amekuwa akipitia wakati mgumu kwa kuwa hana meneja wa kumuwezesha afanye video ya wimbo huo ambao mashabiki wametokea kuupenda.

“Nafanya muziki mzuri lakini ndiyo hivyo sina meneja, nimekosa uongozi wa kuweza kunisimamia nifanye video ya wimbo wangu wa Umeinuliwa, naomba yeyote atakayeguswa anisaidie nikamilishe hii kazi kwa kuwa mashabiki wanaisubiri,” alisema Jordan.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU