KICHUYA ATAMKA KITU KWA OKWI

KICHUYA ATAMKA KITU KWA OKWI

2204
0
KUSHIRIKI

NA ZAINAB IDDY

WINGA wa Simba, Shiza Kichuya, ametamka kitu kimoja kwamba, kulingana na mchuano wa kuwania kiatu cha ufungaji bora msimu huu, anaimani kama hakitakwenda kwa Emmanuel Okwi, basi kitakwenda kwake.

Akizungumza na BINGWA, Kichuya alisema mchuano wa ufungaji bora msimu huu ni mgumu tofauti na msimu uliopita, ndio maana wachezaji wengi walioonekana kung’ara kipindi kilichopita hivi sasa hawapo.

“Ukiangalia kuna sura nyingi mpya katika suala la ufungaji bora wa zamani ni mimi na Mbaraka Yusuph, hii inaonyesha wazi suala la upachikaji wa mabao ni gumu.

“Kwa jinsi hali ilivyo, sina shaka kabisa kuwa Okwi ana nafasi ya kuchukua tuzo hiyo na ikitokea ameshindwa nina hakika itakuwa mali yangu msimu huu,” alisema.

Katika wachezaji wanaowania tuzo baada ya michezo tisa iliyochezwa, Kichuya ana mabao matano sawa na Ibrahim Ajib wa Yanga, wakizidiwa matatu na Okwi aliyecheka na nyavu mara nane hadi sasa.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU