LUKAKU UNANIVURUGA UJUE, MJEZI WAKO MMMH!

LUKAKU UNANIVURUGA UJUE, MJEZI WAKO MMMH!

733
0
KUSHIRIKI

DAAH! Hata sielewi yaani, vitu vingine ni vya ajabu lakini tuyaache hayo bhana. Hivi yule Mayanga anapata wapi ujasiri wa kumweka benchi Ajib pale Stars?

Teh teh teh ina maana hajui kuwa jamaa ameshushwa yule? Miguu yake ina macho yule, anapiga huku na kule. Mara anaitaka tena, ukiingia vibaya tu unapigwa kanzu, halafu tobo. Angalia sasa jinsi anavyoshtua kijoti sasa, teh teh teh!

Ajib hebu niache kwanza aisee. Teh teh teh hivyo vitu vyako kweli umeshushwa asee, ndio maana sikushangaa kabisa kuona umekosa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi sababu hufanani na binadamu wa kawaida. Tuzo yako ndio inatengenezwa baba. Ajib weeee!!

Sasa Mayanga ule ujasiri kautoa wapi jamani? Hadi sasa bado sijaelewa asee, subirini wadau wangu ile nikikutana naye tu n’tamuuliza asee! Hajui kama ule mjezi unatuingizia pesa hapa kwa dobi.

Lakini wakati mwingine tumwache tu, maana alipoingia aliyeshushwa tu wale Benin wote walipaki basi kama lile la Morinyo. Hahaha! kaazi kweli kweli ukiwa fundi basi kazi yako rahisi tu, yaani kukusanya kijiji na kukimbia nacho.

Ule mjezi namba 23 balaa aisee, lakini hata yule Muda mtoto wa yakhee ni hatari asee, pale katikati alivyokuwa anapafanya ni hatari tupu asee, mara kaiweka kwenye taulo, halafu kama anapiga pasi vile kumbe anaminya, ebwanaee Tanzania tumebarikiwa tatizo nini sijui asee au tukamuibe yule Harvey Renard pale Morocco?

Yule kocha fundi bhana, mambo yake sasa anavyofanya ni balaa tupu. Wazambia hawawezi kumsahau asee kwa alichowafanyia mwaka 2012 aliwapa ndoo kwa kuwafunga Ivory Coast kwenye fainali Afcon.

Mwaka 2015 aliwapa ndoo Ivory Coast kwa kuwapiga Ghana kwenye fainali, jamaa anajua sana asee hata sisi tukimchukua huyu itakuwa hatari asee. Tumwachie Mungu tu.

Vitu vingine vinaumiza tu bhana, wakati ule Morinyo kanipigia simu kuhusu Morata n’limwambia hapo sawa asee, sababu yule mtoto anajua bhana.

Si unaona ule mbichwa alioruka mbele ya Bailly pale na kumtungua mikono 100, De Gea. Kumfunga yule kipa inahitajika usiwe na moyo wa binadamu wa kawaida asee.

Morata aliruka kama mwenye mabawa na kupiga kichwa kilichoenda kwenye kona ya mwamba moja kwa moja, huku De Gea akiwa amesimama tu asijue cha kufanya.

Huyo ndio Morata ambaye Morinyo alinipigia simu siku ile, lakini ghafla nikashangaa naambiwa Morinyo kamsajili Lukaku. Jamaa sio mchezaji mbaya lakini inasikitisha asee.

Lukaku alianza ligi kwa moto sana asee, ule mjezi wake hadi kuufua ilikuwa raha asee, povu lilikuwa jeupeee mithili ya theruji kila alipogusa mpira wewe hesabu mpira upo wavuni tu.

Lakini hivi karibuni amekuwa akinivuruga tu, hata sielewi anachofanya asee. Kutuliza mpira imekuwa shida, kukokota imekuwa majaribu kwake, kila anachofanya sasa kimegeuka kuwa uchafu kwake, hakina faida kwake kiasi cha mashabiki wake kumzomea.

Mimi mwenyewe sielewi shida nini asee, wengine wanasema Pogba hayupo, wengine wanasema mbinu za Morinyo zinamfanya aonekane wa hovyo, mi naona wananichanganya tu.

Mjezi wake siku hizi umekuwa mchafu kweli kweli, maji yanatoka machafu sana asee kiasi cha kunifanya nijiulize mara mbili, tatizo nini kwake!

Hakuna namna asee na mimi namwangalia tu sasa hivi maana ushauri wangu hata haufuati. Kila nikimshauri hataki kusikia sasa nami namwacha.

Teh teh teh unajua tangu siku ile niongee na mshkaji wangu alinambia kuwa jinsi Lukaku anavyocheza United, ndio nikaamini kwanini alikuwa chaguo la tatu kwa Morinyo.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU