KIVAZI CHA BEYONCE HARUSI YA SERENA USIPIME

KIVAZI CHA BEYONCE HARUSI YA SERENA USIPIME

430
0
KUSHIRIKI

NEW YORK, Marekani

VAZI alilovaa mwanamuziki, Beyonce wakati wa harusi ya kinara wa tenisi, Serena Williams, linaripotiwa kuwa ndilo lilikuwa kivutio katika sherehe hiyo.

Staa huyo, Beyonce, alikuwa ni mmoja kati ya wageni waalikwa waliohudhuria sherehe hiyo ya ndoa kutokana na kwamba ni rafiki yake wa miaka mingi.

Wakati wa harusi hiyo kimwana huyo anaripotiwa kutinga ukumbini akiwa kwenye gauni la kijani fupi upande mmoja na huku mwingine ukiwa mrefu.

Mbali na vazi pia mwanamama huyo alikuwa amevaa viatu vya wazi vyenye kisigino kirefu, mkufu na hereni ambazo zilionekana kumkaa vyema masikioni.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU