MADONNA AORODHESHWA KWA WAKWEPA KODI

MADONNA AORODHESHWA KWA WAKWEPA KODI

237
0
KUSHIRIKI

LONDON, England

STAA wa muziki wa Pop duniani, Madonna, naye ameripotiwa kuorodheshwa kwenye orodha ya nyota ambao wanakabiliwa na kashfa ya ukwepaji kodi.

Kwa mujibu wa nyaraka zilizovuja  mwishoni mwa wiki iliyopita, staa huyo sambamba na wenzake, Justin Timberlake  na Nicole Kidman, wanaripotiwa kutumia majina yao ili kukwepa kodi katika shughuli ambazo wamekuwa wakizifanya.

Taarifa hizo zinaeleza kuwa nyota hao wamekuwa wakitumia njia tofauti kufungua kampuni katika nchi ambazo sheria za ufuatiliaji kodi hazitiliwi maanani ili kuweza kujilimbikizia kiasi kikubwa kwenye mabenki.

Nyota huyo, Madonna, anakadiriwa kuwa na utajiri wa dola milioni 420 wakati rapa Weinstein, 65 anadaiwa kuwekeza kiasi kikubwa cha fedha kwenye kampuni zilizopo katika kisiwa cha Bermuda na huku pia Madonna akidaiwa mwaka 1998 alinunua hisa 2,000 kwenye Kampuni ya SafeGard Medical Ltd.

Hata hivyo, mwimbaji huyo ambaye jina lake kamili anaitwa Madonna Louise Ciccone, lakini kwenye nyaraka hizo linasomeka kama “Ciccone  Madonna”.

Nyaraka hizo ambazo zilivuja kutoka katika vyombo vya sheria vya kisiwa hicho cha Bermuda, vile vile zinamwonesha Weinstein mwenye utajiri wa pauni milioni 206 mwaka 2001 alinunua hisa  2,000  katika Kampuni ya  Scientia Health Group Ltd.

 

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU