CHEMICAL KUTUMIA ‘DEGREE’ YAKE KWENYE MUZIKI

CHEMICAL KUTUMIA ‘DEGREE’ YAKE KWENYE MUZIKI

601
0
KUSHIRIKI

NA CHRISTOPHER MSEKENA

RAPA mahiri wa kike kwenye muziki wa Bongo Fleva, Claudia Lubao ‘Chemical’, amesema shahada yake ya kwanza ya sanaa na ubunifu aliyoipata wiki hii katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ataitumia kuboresha tasnia nzima ya muziki.

Akizungumza na Papaso la Burudani, Chemical alisema masomo yalikuwa yanambana na kufanya apoteze baadhi ya vitu lakini hivi sasa amemaliza na yupo tayari kuwatumikia mashabiki zake.

“Najisikia vizuri kumaliza ‘degree’ yangu niliyokuwa nachukua kwa miaka mitatu inayohusu sanaa na ubunifu, nilikuwa napata tabu kuchanganya masomo na muziki lakini hivi sasa nimemaliza na nitatumia elimu yangu kufanya vitu vikubwa na tofauti ambavyo wengi walikuwa wanatamani kuviona kwenye muziki wetu,” alisema Chemical.

 

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU