DK. SHIKA ANOGESHA KIBA-100 YA ROSTAM

DK. SHIKA ANOGESHA KIBA-100 YA ROSTAM

778
0
KUSHIRIKI

NA CHRISTOPHER MSEKENA

STAA mpya kwenye tasnia ya burudani Bongo, Dk. Louis Shika, ameendelea kupata dili baada ya kunogesha video mpya ya Rostam (Roma Mkatoliki na Stamina) waliomshirikisha Maua Sama inayoitwa Kiba-100, iliyotoka juzi.

Akizungumza na Papaso la Burudani, Stamina alisema umoja wao (Rostam), umedhamiria kuendelea kudondosha burudani kwa mashabiki ndiyo maana baada ya kutoa, Hivi Ama Vile, wameibuka na Dk. Shika kwenye ngoma yao mpya, Kiba_100.

“Mzigo (video) tayari upo YouTube na tunashukuru kwa kuwa ndani ya saa nane tumeweza ku-trend hadi namba 1, Dk. Shika ndiye staa mpya mjini, tukaona si vibaya akiwepo kwenye ngoma yetu,” alisema Stamina.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU