LULU DIVA: SITATUMBUIZA ILA NITAKUWEPO FIESTA

LULU DIVA: SITATUMBUIZA ILA NITAKUWEPO FIESTA

351
0
KUSHIRIKI

NA CHRISTOPHER MSEKENA

UFUATIA ufinyu wa muda uliopelekea baadhi ya wasanii kutotumbuiza kesho kwenye tamasha la Fiesta akiwemo, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’, msanii huyo amesema atahudhuria kuwatazama mastaa wengine wakiangusha burudani.

Staa huyo wa singo ya Utamu, ameliambia Papaso la Burudani kuwa ilikuwa ni ndoto yake kutumbuiza kwenye kilele cha tamasha hilo linalofanyika kesho kwenye viwanja vya Leaders Club, lakini muda umeyeyusha ndoto zake.

“Nimepokea kwa huzuni taarifa za kutotumbuiza kwa sababu muda umepunguzwa mpaka saa 6 usiku, lakini nitakwenda kutazama wasanii wenzangu wanafanya nini, Serikali inapaswa kuliangalia hili kwa sababu mfano mimi ningetumbuiza nyuma yangu kuna vijana wengi wangepata ajira kupitia mimi, lakini mimi nimekosa na wao pia wamekosa ajira,” alisema Lulu Diva.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU