DULLY SYKES AFUNGUKA ‘BOMBARDIER’ ILIVYOFANYIKA

DULLY SYKES AFUNGUKA ‘BOMBARDIER’ ILIVYOFANYIKA

411
0
KUSHIRIKI

 

NA CHRISTOPHER MSEKENA

MKONGWE wa muziki wa Bongo Fleva, Dully Sykes, amesema wimbo wake mpya, Bombardier aliyoiachia hivi karibuni ilifanyika ndani ya siku saba mpaka kukamilika.

Akizungumza na Papaso la Burudani, Dully Sykes, licha ya kuogopa kupanda ndege, ndani ya wimbo huo amejifananisha na ndege hizo aina ya Bombardier zenye uwezo wa kuruka juu umbali mrefu na kukaa angani kwa saa 16-18.

“Wimbo ulifanyika kwa siku saba mpaka kuwafikia mashabiki, Mr T Touch alinitumia biti, siku ya pili nikaenda studio kwake kurekodi, siku ya tatu akanitumia wimbo ukiwa umekamilika na siku hiyo hiyo nikamtumia director Deo Abel, siku iliyofuata tukafanya video na siku mbili mbele video ikatoka,” alisema Dully Sykes.

Aliongeza kwa kuwaomba mashabiki zake kuingia kwenye mtandao wa YouTube na kuiangalia video ya Bombardier.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU