‘JANUARY TO DECEMBER’ YA HEMEDY PHD FUNGA MWAKA

‘JANUARY TO DECEMBER’ YA HEMEDY PHD FUNGA MWAKA

528
0
KUSHIRIKI

 

NA SHARIFA MMASI

MSANII wa filamu na muziki nchini, Hemed Suleiman ‘Hemedy PhD’, amesema mapokezi makubwa ya wimbo wake mpya, ‘January To December’ yamefanya kazi hiyo iwe ya mwisho kwake mwaka huu.

Hemedy PHD, alisema wimbo huo ambao ameutoa siku tatu zilizopita umepokewa vizuri kiasi cha kuimbwa na watu mbalimbali hata watoto kwenye mitaa mbalimbali.

“January To December’ ni ngoma yangu mpya niliyoiachia hivi karibuni, namshukuru Mungu imepata mapokezi ya aina yake yanayoendelea kuniweka kwenye chati ya mastaa wakali Afrika Mashariki na Kati, natoa wito kwa mashabiki zangu kutembelea tovuti ya mkito.com kuupakua,” alisema Hemedy.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU