ADELE HANA WIMBO MIAKA MIWILI NA MPUNGA UNAINGIA

ADELE HANA WIMBO MIAKA MIWILI NA MPUNGA UNAINGIA

290
0
KUSHIRIKI

LONDON, England

MWANAMUZIKI wa England, Adele, ameripotiwa kuvuna kiasi cha pauni milioni tisa kwa mwaka licha ya kutokuwa na wimbo mpya tangu 2015.

Mkali huyo mwenye sauti maridhawa, mwenye albamu tatu zinazotamba pamoja na tuzo 15 za Grammy’s, anaonekana kupokea kiasi kikubwa cha fedha kwa mwaka licha ya kwamba hana kazi kubwa aliyoifanya ndani ya miaka miwili zaidi ya kulea familia.

Kwa mujibu wa mtandao wa Daily Mirror, fedha hizo zinaendelea kupatikana kutokana na mauzo ya albamu yake ya ‘25’ aliyoiachia Novemba 2015.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU