AZAM WAFUNGA USAJILI DIRISHA DOGO

AZAM WAFUNGA USAJILI DIRISHA DOGO

844
0
KUSHIRIKI

NA TIMA SIKILO

UONGOZI wa klabu ya Azam FC, umeweka wazi kuwa umekamilisha  usajili wake katika dirisha dogo msimu huu, hivyo hauhitaji kuongeza mchezaji mwingine.

Azam imekamilisha usajili waka baada ya kunasa saini ya mshambuliaji wa kigeni kutoka nchini Ghana, Bernard Arthur pamoja na kumuongezea mkataba wa mwaka mmoja Mzimbabwe, Bruce Kangwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Ofisa habari wa klabu hiyo, Jaffar Idd, alisema zoezi la usajili limekamilika kulingana na ripoti ya kocha wa timu hiyo, Aristica Cioaba.

“Kwa mujibu wa ripoti, wachezaji waliotakiwa ni wawili wa kimataifa  ambapo Arthur na Kangwa tayari  wameshasajiliwa, wachezaji wazawa waliopo wanatosha,” alisema.

Aliongeza kuwa, baada ya Ligi Kuu Tanzania Bara kusimama wametoa  mapumziko ya muda mfupi kwa wachezaji kabla ya kurejea kambini na kuendelea na maandalizi.

Wakati huo huo, Jaffar alimtangaza Himid Mao kuwa ndiye mchezaji bora wa timu hiyo kwa Oktoba, baada ya Yakubu Mohamed na Mbaraka Yussuf kuchukua miezi miwili iliyopita.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU