KIMENYA AITAKA AZAM, AZIGOMEA SIMBA, YANGA

KIMENYA AITAKA AZAM, AZIGOMEA SIMBA, YANGA

1407
0
KUSHIRIKI

NA WINFRIDA MTOI

BEKI wa Tanzania Prisons, Salum Kimenya, amefunguka na kuweka wazi kuwa timu inayoweza kumshawishi kuachana na ajira yake ni Azam FC pekee, lakini si Simba wala Yanga.

Tangu msimu uliopita beki amekuwa akihusishwa kujiunga na vigogo hao wa soka nchini lakini hadi sasa hakuna klabu iliyoweka mezani dau analohitaji mchezaji huyo.

Akizungumza na BINGWA jana, Kimenya ambaye anahitaji zaidi ya Sh milioni 80 ili aachane na ajira yake katika Jeshi la Magereza, alisema  kinachomvutia kucheza Azam ni malengo ya klabu hiyo pamoja na kujali wachezaji.

Alisema bado ana muda mrefu wa kucheza soka, hivyo kama ataondoka Prisons ni lazima ajiunge na timu ambayo itamhakikishia kuendeleza kipaji chake.

“Nazisikia sana hizo taarifa za kwamba natakiwa na Simba mara Azam, lakini ukweli ni kwamba hakuna kiongozi hata  mmoja nimefanya naye mazungumzo. Lakini kama ni kweli basi timu ninayopenda kucheza ni Azam,” alisema Kimenya.

Alieleza kuwa Simba anaweza kucheza wakikubaliana lakini kwa masharti ya kumhakikishia juu ya maisha yake ya soka ndani ya timu hiyo.

Alisema hataki kusajiliwa na kuchukua fedha  halafu mwisho wa siku anakosa namba ya kucheza na kupoteza kipaji chake.

 

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU