MAJIMAJI MBIONI KUMREJESHA KIDUKU

MAJIMAJI MBIONI KUMREJESHA KIDUKU

912
0
KUSHIRIKI

NA WINFRIDA MTOI

KLABU ya soka ya Majimaji ipo mbioni kumrejesha kikosini mshambuliaji, Kelvin Sabato ‘Kiduku’ anayekipiga Mtibwa Sugar kwa sasa, baada ya Marcel Kaheza kutaka kutimkia Singida United.

Kiduku alijiunga na kikosi cha Majimaji msimu uliopita akitokea Stand United ya mkoani Shinyanga, lakini alicheza kwa muda mfupi.

Rafiki wa karibu wa mchezaji huyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini, aliliambia BINGWA kuwa, straika huyo ameuomba uongozi wa Majimaji kurejea kikosini hapo.

Naye Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Zacharia Ndumbaro, licha ya kutotaja jina la Kiduku, alikiri kuwa wapo kwenye mazungumzo na klabu moja ili waweze kumpata straika aliyependekezwa na kocha katika ripoti yake.

“Kwa mujibu wa mapendekezo ya kocha, tunahitaji kusajili straika mwingine ambaye tayari tumeanza naye mazungumzo na tukimalizana  naye tutaweka hadharani,” alisema.

Wakati huo huo, uongozi wa Majimaji ulitarajia kukutana na viongozi wa klabu ya Singida United jana ili kuzungumzia  suala la mshambuliaji wao Kaheza  ambaye wanamuhitaji.

 

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU