MTIBWA: HATUNA MPANGO WA KUSAJILI

MTIBWA: HATUNA MPANGO WA KUSAJILI

678
0
KUSHIRIKI

NA MAREGES NYAMAKA

KLABU ya soka ya Mtibwa Sugar haina mpango na usajili wa dirisha dogo linaloendelea kwa timu za Ligi Kuu Tanzania Bara, kutokana na kocha wao, Zuberi Katwila, kuweka wazi kuwa hahitaji kuongeza wachezaji wapya.

Akizungumza na BINGWA, Katwila alisema ana kikosi kipana ambacho kimeimarika kila idara ndio maana  hafikirii kufanya usajili katika dirisha dogo.

Alieleza kuwa anaweza kusajili iwapo  baadhi ya wachezaji waliopo sasa wataondoka na kuacha pengo katika  kikosi hicho.

“Sina matarajio ya kusajili kwa sababu  nawaamini wachezaji waliopo kwani  wengi ni vijana na baadhi yao bado hawajapata nafasi ya kucheza,” alisema Katwila.

Wachezaji waliosajiliwa katika dirisha kubwa lililofungwa Agosti 6, mwaka huu ni Hassan Isihaka kutoka African Lyon, Hassan Dilunga (JKT Ruvu) na Kelvin Sabato (Majimaji).

Kikosi cha Mtibwa kinashika nafasi ya tano katika msimamo wa ligi kuu, baada ya kufikisha pointi 18  huku Simba wakiwa kileleni kwa idadi ya mabao mengi, lakini wakiwa na pointi 23 sawa na Azam.

 

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU