MWADUI KUZIBOMOA KAGERA, MBEYA CITY

MWADUI KUZIBOMOA KAGERA, MBEYA CITY

766
0
KUSHIRIKI

NA WINFRIDA MTOI

KLABU ya Mwadui FC inawafukuzia wachezaji wawili kutoka timu za Mbeya City na Kagera Sugar, kwa ajili ya kuimarisha kikosi hicho katika usajili wa dirisha dogo.

Habari za uhakika kutoka kwa kiongozi mmoja wa klabu hiyo zinadai kuwa, ripoti ya kocha wa timu hiyo, Jumanne Ntambi, imeainisha majina ya wachezaji wanaohitajika akiwamo Eliud Ambokile wa Mbeya City.

Ripoti ya kocha pia imependekeza kusajiliwa washambuliaji wawili akiwamo kinara wa mabao katika timu ya Majimaji na kiungo kutoka Kagera Sugar.

Akizungumza na BINGWA, Ambokile alisema hana taarifa za kutakiwa na Mwadui labda uongozi wa timu yake ndio unafahamu kwa sababu bado ana mkataba na klabu hiyo.

“Sijafanya mazungumzo yoyote na Mwadui kwa sababu bado nina mkataba wa mwaka mmoja na Mbeya City, pia ninahitaji kuendelea kuichezea timu yangu,” alisema Ambokile.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU