INIESTA KUIKOSA SPORTING

INIESTA KUIKOSA SPORTING

113
0
KUSHIRIKI

BARCELONA, Hispania

KLABU ya Barcelona imesema kwamba, Andres Iniesta, hatakuwamo katika mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Sporting CP kutokana na majeraha ya kiazi cha mguu yanayomkabili.

Staa huyo mwenye umri wa miaka 33, alipumzishwa dakika ya 53 ya mchezo huo uliopigwa mwishoni mwa wiki iliyopita na nafasi yake ikachukuliwa na Denis Suarez.

Timu hizo zilishindwa kutambiana baada ya kwenda sare ya kufungana mabao 2-2 dhidi ya Celta Vigo wakiwa katika Uwanja wa Camp Nou.

Baada ya kufanyiwa vipimo ilibainika kwamba nahodha huyo ana matatizo hayo kwenye misuli ya kiazi hicho cha mguu na hivyo atakuwa nje ya uwanja wakati Barca wakiwavaa Wareno hao.

Barca tayari wameshakata tiketi ya kucheza hatua ya mtoano kupitia Kundi D, lakini Sporting wanaweza kushika nafasi ya pili endapo wataondoka Camp Nou wakiwa na ushindi na huku Juventus wakishindwa kuifunga Olympiacos.
Katika mchezo wa kwanza vinara hao wa Catalans walishinda 1-0 wakiwa ugenini mjini Lisbon.

HAKUNA MAONI