MATIBABU YA KAMUSOKO ACHA KABISA

MATIBABU YA KAMUSOKO ACHA KABISA

1767
0
KUSHIRIKI

NA TIMA SIKILO

THABAN Kamusoko anafanyiwa matibabu ya nguvu chini ya jopo la madaktari linaloongozwa na daktari wa zamani wa Yanga, Nassor Matuzya katika hospitali ya Temeke.

Kamusoko ambaye ana majeraha kwenye goti lake, amelazimika kukosa baadhi ya michezo ndani ya kikosi chake cha Yanga na sasa madaktari wenye ushabiki na klabu hiyo wameamua kulivalia njuga ili arudi mapema uwanjani.

Akizungumza na BINGWA, Dk. Matuzya alisema hali ya Kamusoko kwa sasa inaendelea vizuri na baada ya wiki mbili anaweza kuanza mazoezo mepesi kwani tiba anayopewa ni nzuri.

“Kwa sasa hali ya Kamusoko ni nzuri na anaendelea na matibabu, kama atatumia dawa inavyotakiwa na kufuata ushauri wa madaktari, basi baada ya wiki mbili anaweza kuwa fiti na kuanza mazoezi mepesi ya kutembea kwa kasi,” alisema Matuzya.

Alisema kwa kuwa mchezaji huyo ameshapata matibabu, hakuna haja ya kumharakisha kumrejesha uwanjani na badala yake aachwe apone taratibu.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU