MSUVA AZIDI KUNG’ARA MOROCCO

MSUVA AZIDI KUNG’ARA MOROCCO

774
0
KUSHIRIKI

NA SALMA MPELI

WINGA wa Kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva, amezidi kung’ara katika Ligi Kuu nchini Morocco, baada ya kutupia mabao ambapo hadi sasa ameshaifungia timu yake ya Difaa el Jadida jumla ya mabao matatu.

Msuva ambaye ni winga wa zamani wa Yanga, alijiunga na timu hiyo mwanzoni mwa mwaka huu, kwa mkataba wa miaka mitatu.

Katika timu yake hiyo mpya, Msuva yupo nafasi ya tatu kwenye orodha ya wafungaji, huku wakiongozwa na Bilal el Megri na Hamid Ahaddad wenye mabao matano kila mmoja.

Difaa iliibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya timu ya Olympique Khouribga katika mchezo wa ligi hiyo, huku Msuva akifunga bao moja kwenye ushindi huo wa mabao manne.

Katika ligi hiyo inayojulikana kama Botola Pro, Difaa ipo kwenye nafasi ya pili ikiwa na jumla ya pointi 17 na mabao 18 ya kufunga katika msimamo wa ligi hiyo inayoongozwa na Hassania Agadir ikiwa na pointi 19.

Katika orodha ya wafungaji wa jumla kwenye ligi hiyo, Msuva yupo kwenye nafasi ya 14.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU