NGOMA KUPIGWA BEI

NGOMA KUPIGWA BEI

3220
0
KUSHIRIKI

THOMAS NG’ITU NA HUSSEIN OMARY

HATIMAYE mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma, amewekwa sokoni na timu yoyote itakayoweka dau la maana inaweza kumchukua mchezaji huyo wa Zimbabwe.

Taarifa za kutoka ndani ya klabu ya Yanga, zinasema kuwa kama Ngoma atasalimika kwenye dirisha hili dogo la usajili, basi msimu ujao lazima ataondoka kwenye klabu hiyo inayotumia jezi za rangi ya kijani na njano.

Ngoma amekuwa kwenye mzozo mkubwa na Yanga baada ya kwenda kwao Zimbabwe bila kuutaarifu uongozi wa klabu hiyo ambayo inapambana kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, jambo ambalo limesababisha baadhi ya mashabiki kuanza kumchukia.

Chanzo cha ndani kimesema baada ya mchezaji huyo kutua nchini wiki iliyopita, unafanyika mpango wa kumweka kiti moto ili atoe utetezi wake kuhusiana na  uamuzi wake wa kuondoka bila kuuaga uongozi wa klabu hiyo ya Yanga.

Wakati uongozi huo wa Yanga ukitarajia kukaa na Ngoma, kocha George Lwandamina alishaweka wazi kwamba hamhitaji mshambuliaji huyo kutokana na utovu wake wa nidhamu.

Kigogo mmoja ndani ya klabu hiyo ameliambia BINGWA, kuwa Ngoma hatakuwa na maisha marefu kwenye timu hiyo na badala yake atauzwa kwingine hata kama isiwe katika dirisha hili dogo.

“Kwa hali ilivyo ni kwamba Donald Ngoma hatakuwa na maisha marefu kwenye timu, licha ya kwamba aliongeza mkataba wa miaka miwili, lakini kwa jinsi mambo yanavyokwenda ataondoka hata kama isiwe dirisha hili dogo la usajili,” alisema kigogo huyo.

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU