RAIS MADRID AMPA RONALDO BALLON D’OR

RAIS MADRID AMPA RONALDO BALLON D’OR

144
0
KUSHIRIKI

MADRID, Hispania

RAIS wa timu ya Real Madrid, Florentino Perez, ametangaza kwamba staa wao, Cristiano Ronaldo, ndiye atakayenyakua tuzo ya mchezaji bora wa dunia, Ballon d’Or  na si hasimu wake,  Lionel Messi.

Mreno huyo ambaye mwezi uliopita alifanikiwa kutwaa tuzo hiyo kwa upande wa wanaume, pia anapewa nafasi ya kukabidhiwa mzigo huo baada ya mwaka huu kuiwezesha Real Madrid kutwaa ubingwa wa La Liga na wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Lakini kuna tetesi zinazodai straika wa  Barcelona, Messi, ndiye atakayetangazwa kuwa mshindi kesho kutwa, baada ya jarida moja nchini Ufaransa kumwonesha nje ya jalada lake akiwa ameshika tuzo hiyo.

Hata hivyo, taarifa kutoka nchini Hispania, zinaeleza tayari Ronaldo ameshapewa taarifa kwamba atatwaa tuzo hiyo na huku Messi akiwa ameshapewa pongezi kwa mafanikio yake jambo ambalo linamfanya Perez  kuonekana hana shaka katika hilo.

“Ronaldo ni moja ya kielelezo kikubwa,” alisema  rais huyo akiwa mjini Madrid. “Katika historia yetu ndiye anayeongoza kwa ufungaji. Siku chache zilizopita ndiye aliyetwaa tuzo hiyo na sasa anaelekea kuchukua ya Ballon d’Or kwa mara ya tano.”

HAKUNA MAONI

ACHA JIBU